Pages

Thursday, June 2, 2011

AHADI ZA KIKWETE- 2010 - 2015


1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ngombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Monday, May 30, 2011

Bilioni 113 zakwamisha Bajeti ya Uchukuzi

KAMATI ya Bunge ya Miundombinu, imeikataa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi hadi serikali itakapowasilisha kiasi cha Sh113 bilioni za bajeti ya mwaka wa fedha unaoisha Juni 31, mwaka huu. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba alisema serikali haikuwasilisha fedha zote zilizoombwa na wizara hiyo ambazo zilikuwa ni Sh95 bilioni na badala yake iliwasilisha Sh45 bilioni hadi Machi, mwaka huu.

Alisema wahisani walitoa Sh65 bilioni katika bajeti hiyo lakini hadi Machi, mwaka huu ni Sh2bilioni tu ambazo zilikuwa zimewasilishwa katika wizara hiyo. Alisema fedha hizo zingetosha kuboresha miundombinu nchini ikiwamo barabara (kwa kiwango cha lami) viwanja vya ndege na reli. “Yaani inachekesha kwa kweli, leo tunapitisha Bajeti ya Serikali wakati iliyopita pesa haikufika kama ilivyotakiwa! Sasa tunapitisha bajeti ya nini? Lazima ikwame tutakutana huko Bungeni zitolewe ufafanuzi hizi pesa,” alisema Serukamba.

Mwenyekiti huyo alisema ili bajeti hiyo ipite ni lazima serikali itoe fedha za kufufua miundombinu kwanza ambazo ni pamoja na Sh1.6 bilioni kwa ajili ya kuboresha usafiri wa meli, Sh23 bilioni kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na Sh 241 bilioni ziende Shirika la Reli Tanzania (TRL).

Serukamba ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), alisema serikali haiko makini kwa sababu haitoi kipaumbele kwa bajeti ya uchukuzi. Alisema nchi yoyote yenye maendeleo duniani lazima itoe kipeumbele katika miundombinu ili ifanye kazi ya kusafirishia bidhaa mbalimbali za kukuza uchumi. “Hakuna nchi yenye maendeleo ambayo haina barabara, reli, anga, bandari za uhakika za kusafirishia mazao na mengineyo kwa ajili ya uchumi wa nchi.”

Alisema mapendekezo ya bajeti hiyo ambayo yaliwasilishwa mbele ya kamati yake kwa mwaka 2011/2012, ilikuwa na upungufu hivyo kulikuwa hakuna sababu za kuipitisha. Alisema serikali ina fedha za kutosha lakini akashangaa kuona ATCL linakufa huku likiwa linaangaliwa kama ilivyo kwa TRL ambalo nalo linasuasua. Serukamba alimwambia Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu kuwa serikali inatakiwa kujipanga tena kwa makini kuliokoa taifa kiuchumi. Alisema inawezekana wizara hiyo ikawa na malengo mengi mazuri lakini yakakwamishwa na bajeti inayopatiwa na Hazina.

“Sitashangaa kwani leo tumemsikia waziri hapa akieleza malengo mengi ambayo wanataraji kuyafanya lakini sasa watayafanyaje ikiwa hakuna fedha za kutosha," alisema. Awali, Waziri Nundu alisema katika jitihada za kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, wizara yake kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imeendelea kuhimiza matumizi ya mabasi makubwa tu kutoa huduma katikati ya jiji, hatua ambayo kwa kiasi kikubwa imepunguza tatizo. Wabunge wahoji hatima ya ATCL

Wabunge wa Kamati hiyo walitaka kujua hatima ya ATCL wakisema licha ya kutofanya kazi, bado wafanyakazi wake wanalipwa mishahara. Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali aliitaka serikali kueleza wafanyakazi hao watalipwa mishahara mpaka lini wakati shirika lenyewe halifanyi kazi kwa muda mrefu sasa.

Alisema ingekuwa vizuri Waziri Nundu aeleze kiundani suala la wafanyakazi hao kulipwa mishahara na inakotoka. Pia alitaka kujua ni lini serikali italifufua tena shirika hilo kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa nchi ambao umeshuka kwa kasi baada ya kufa kwake.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Mohamed Mnyaa alisema ni vigumu kusikia wafanyakazi wanalipwa mishahara mpaka leo wakati shirika lenyewe limeshakufa. Akijibu hoja hiyo Waziri Nundu alisema katika jitihada za kuinusuru ATCL, serikali imekuwa ikilipa mishahara ya wafanyakazi na fedha za matengenezo ya ndege. Alisema serikali bado ipo katika jitihada za kulifufua shirika hilo ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo na wawekezaji mbalimbali.

Tuesday, April 12, 2011

Babu kusitisha huduma Pasaka

MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila, ametangaza kuwa hatatoa huduma ya tiba siku za Ijumaa Kuu na Jumapili ya Pasaka.Mchungaji huyo alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Samunge, Loliondo, wilayani Ngorongoro.

"Huduma itasitishwa Ijumaa Kuu yaani Aprili 22 na Jumapili ya Pasaka, Aprili 24 na itaendelea Aprili 23 na Aprili 25 baada ya Pasaka," alisema.

Mchungaji Mwasapila amewataka wagonjwa wanaopanga kwenda kupata tiba kwake wakati wa Sikukuu ya Pasaka kuangalia ratiba yake hiyo ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima.

Katika hatua nyingine, mgogoro wa mapato yanayotokana na wagonjwa wanaokwenda kupata tiba kwake, umechukua sura mpya baada ya Halmashauri ya Kijiji cha Samunge kupitisha uamuzi wa kuanza kukusanya ushuru wake mbali na kuzuiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.

Kijiji hicho kimesema sasa kitatoza ushuru wa Sh2,000 kwa kila gari linalofika kwa Mchungaji huyo huo ukiwa ni mbali na ule wa Sh5,000 unaotozwa na Halmashauri ya Wilaya.

Katika kikao kilichofanyika jana hapa Samunge, pia wajumbe kwa kauli moja walipinga uamuzi wa Halmashauri ya Ngorongoro na Serikali Kuu kuingilia masuala ya maendeleo ya kijiji chao bila ya kuwashirikisha.

Akitangaza uamuzi huo jana, Diwani wa Kata ya Samunge, Jackon Sandea alisema wataanza kukusanya ushuru mara tu baada ya kupata idhini ya Mkutano Mkuu wa Kijiji utakaofanyika kesho na kufuatiwa na kikao cha maendeleo Kata ya Samunge.

"Tumekubaliana halmashauri wao wakusanye hizo Sh5,000 zao na sisi tutaanza kukusanya zetu Sh2,000 kwani, Mchungaji Ambilikile yupo kijijini kwetu na sisi ndiyo tunaopata adha ya kupokea maelfu ya wageni na siyo wilayani au mkoani," alisema Sandea na kuongeza:

"Wao wameleta barua ya taarifa tu kutaka sisi tusichukue ushuru lakini, hatujawahi kukaa pamoja na kushauriana na tunaona uamuzi wao huu ni kuingilia mamlaka halali ya kijiji."

Alisema wanashangaa kuona Serikali Kuu inataka tena ipewe Sh3,000 kwa kila gari wakati tayari inakusanya fedha za ukaguzi wa magari yote yanayokwenda Samunge, na fedha za kutoa vibali.

Uamuzi huo wa kijiji kutaka kuchukua ushuru huenda ukaibua mgogoro mkubwa wakati wa kukusanya mapato kwani tangu April 6 mwaka huu, watendaji wa halmashauri hiyo walipoanza kukusanya ushuru wa Sh5,000 na kuwatimua wakusanya ushuru wa kijiji hicho.

Aomba waliokwama Bunda waruhusiwe
Katika hatua nyingine, Mchungaji Mwasapila, ameiomba Serikali kupunguza masharti kwa watu waliokwama katika Mji wa Bunda, mkoani Mara ili waweze kufika Samunge kupata tiba.

Akizungumza na Mwananchi kwa niaba ya Mchungaji Mwasapila, Msaidizi wake, Fred Nsajile alisema wamepata taarifa za mamia ya watu kuendelea kukwama wilayani Bunda kutokana na utaratibu wa kuruhusu magari kuwa mgumu.

"Mchungaji anaomba watu wanaopitia Bunda waruhusiwe kwa wingi kuliko maeneo mengine kwani eneo hilo linatumiwa na mikoa mitano na watu kutoka nje ya nchi," alisema
Jana wagonjwa wanaliozuiwa katika Kituo cha Bunda walifunga barabara kuu ya Mwanza-Musoma kwa saa kadhaa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wakishinikiza kufunguliwa kwa kizuizi hicho.

Tukio hilo limetokana na jazba iliyosababishwa na kifo cha mgonjwa mwenzao, aliyefariki dunia juzi baada ya kucheleweshwa kituoni hapo kuendelea na safari.

Mgonjwa huyo mwanamume ambaye hadi sasa hajatambulika jina lake mkazi wa Kijiji cha Kakola, wilayani Kahama, Shinyanga alifariki juzi majira ya saa tisa alasiri.

Tukio hilo la kufunga barabara limekuja siku mbili tu baada ya wagonjwa hao kufanya hivyo Ijumaa iliyopita. Hata hivyo, Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha Jeshi la Polisi kiliwatawanya watu hao baada ya kukaa hapo kwa takriban saa mbili.

Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wagonjwa hao walisema waliamua kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe wao kwa Serikali.

Wageni waongezeka Samunge

Foleni ya magari yanayopeleka wagonjwa kwa Mchungaji Mwasapila juzi na jana iliendelea kuongezeka na kufikia takriban kilometa 10.

Kuongezeka kwa magari kulitokana na dawa kumalizika mapema Jumamosi wiki iliyopita na kuchelewa kuanza kwa utoaji wa dawa siku ya Jumapili utoaji wa dawa ulichelewa kuanza.

Idadi ya watu kutoka nje ya nchi wanaokwenda kupata tiba Samunge imekuwa ikiongezeka sasa na wengi wanatoka nchi jirani ya Kenya na nchi za Ulaya.

Jana wageni kadhaa kutoka Uingereza waliongozwa na Colin Higgins walitua Samunge na ndege ndogo na kupata kikombe cha dawa. Higgins ambaye ni mfanyabiashara wa magari ya mafuta mkoani Morogoro, alikuwa ameambatana na Grain Mcdonald. Donald Mcdonald, Niel Mcdonald na Watanzania, Annie Voltaire na Dorothy Sen.

source mwananchi

Viongozi wa vyama vya siasa, dini wazungumzia CCM kujivua gamba

Vyama vya siasa vimesema hatua ya CCM kujivua gamba haitasaidia kukijenga chama hicho iwapo viongozi wapya wa chama hicho wataendelea kuwa na tabia na hulka za zamani.

Wengine wamemshauri Rais Jakaya Kikwete avunje pia Baraza la Mawaziri, kwani huko ndiko kwenye udhaifu mkubwa wa kiutendaji kuliko kwenye chama.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema litakuwa jambo jema kama CCM imejivua gamba kwa ajili ya kuleta mabadiliko na si kuwa kizingiti cha mabadiliko.

Alisema walichofanya CCM ni jambo la kawaida kila baada ya uchaguzi vyama vimekuwa vikikaa na kuangalia upungufu uliojitokeza na kisha kufanya mabadiliko kujiimarisha.

Profesa Lipumba alisema CCM imekaa madarakani miaka 50, hivyo ni dhahiri inahitaji kufanya mabadiliko makubwa kwa kuwa hivi sasa imepoteza dira na mwelekeo kutokana na kushindwa kutatua kero za wananchi.

Alisema kujivua kwake gamba kusaidie kuleta tume huru ya uchaguzi na kuwezesha mabadiliko ya kuanzishwa kwa katiba mpya.

Kujivua gamba kwa CCM kutakuwa kuzuri kama watawezesha kufanyika kwa mabadiliko. Ila kama wanajivua gamba kwa ajili ya kuzuia mabadiliko watajiweka pabaya, watu wanataka mabadiliko,” alisema.

Mwenyekiti wa APPT Maendeleo, Peter Mziray, alisema CCM imebaini kuwa kuna ushindani mkubwa wa kisiasa na ndiyo sababu imeaanza kupapatika.

Alisema kinachokiumiza chama hicho, ni ufisadi kama walivyokiri wenyewe na kwa kuwa mafisadi wengi wanatoka chama hicho lazima wajisafishe kama wanataka wananchi wawaamini.

Aliongeza kuwa CCM lazima ikubali kuwa imechoka na kuzeeka na haijaja na ajenda mpya ya kuwashawishi Watanzania kuendelea kuwaamini na haiwezi tena kutawala nchi.

Alisema iwapo CCM itajichanganya na kuteua Katibu Mkuu asiye mwanasiasa itakuwa inajichimbia kaburi kwani kwa hali ilivyofikia chama hicho hakirekebishiki tena.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, alisema CCM kujivua gamba ni sawa na janja ya nyani kwa kuwa nyoka ni yule yule na Watanzania wasitarajie mabadiliko makubwa.

Alisema serikali ya CCM inapaswa kuamka na kuhakikisha inaondoa pengo kati ya maskini na matajiri kwa kuwa limekuwa kubwa na kusababisha umaskini kuzidi kuongezeka.

Mbatia alisema CCM haina itikadi hadi sasa kwani ujamaa waliokuwa wakiuhubiri zamani walishautelekeza na kukumbatia mafisadi, ambao ndio wameifikisha Tanzania katika lindi la umaskini.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, alisema kuvunjwa kwa sekretarieti ya CCM na CC na Makamba hakutasaidia sana kwa kuwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi waliotajwa na chama hicho bado wako serikalini.

Alisema hatua ya watuhumiwa hao kuwa wajumbe wa vikao nyeti vya Kikatiba, kunaonyesha namna gani viongozi wa CCM wasivyo makini na kwamba, hali hiyo ndiyo inawafanya wananchi wapoteze imani na chama hicho.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alisema hata CCM ingejivua magamba kumi na ikajichuna hadi ngozi, haiwatishi na wataendelea kupambana nao hadi wang’oke madarakani.

Alisema kimsingi Chadema kinafurahi iwapo CCM itazidi kuimarika kwani kushindana na chama dhaifu haitakuwa jambo la maana kwao.

Mimi sioni wamejivua gamba kwa namna gani. Mabadiliko haya tunayaona kila siku. Lakini watu ni wale wale na tabia zile zile. Binafsi nafurahia mabadiliko ya CCM. Nataka tupambane na chama imara,” alisema.

Sheikh wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum, alisema sekretarieti mpya ya CCM iliyoundwa, ni timu nzuri.

Alisema anaamini inaweza kuleta mabadiliko makubwa na kurejesha heshima kwa chama hicho iliyoanza kupotea.

Sheikh Alhad alisema hayo alipozungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE jana.

Uzoefu wao katika chama na serikali naujua. Uwajibikaji wa Mukama, ni mchapakazi sana na wote wengine,” alisema Sheikh Alhad.

Alisema jambo lingine linalompa matumaini juu ya watendaji hao wapya wa CCM, ni kutokana na kutokuwa na makundi, ambayo alisema ni tatizo kubwa lililokuwa likikitafuna chama hicho.

CHANZO: NIPASHE

Chenge, Rostam watoswa rasmi

Kama ni kujivua gamba, basi mchakato huo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulianza jana baada ya makada wake mashuhuri, Andrew Chenge na Rostam Aziz, kuondolewa rasmi katika nafasi za ujumbe wa Kamati Kuu (CC).

Mabadiliko hayo yamefuatia kujiuzulu kwa Sekretarieti na wajumbe wa kuchaguliwa wa CC Jumamosi iliyopita ukiwa ni mkakati ulioelezwa kuwa unalenga kufanya mageuzi makubwa ndani ya CCM.

Wengine ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Kuu iliyojiuzulu na hawakurudi katika mchujo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, aliyekuwa Katibu wa Ushirikiano wa Mambo ya Nje. Mwingine ni Margaret Sitta.

Katika uchaguzi uliofanyika jana wakati wa kikao cha siku mbili cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, wajumbe waliochaguliwa kuunda CC mpya kutoka Zanzibar ni: Samia Suluhu ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano); Dk. Hussein Mwinyi ambaye pia ni waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Mwanasiasa mkongwe na mbunge wa viti maalum, Dk. Maua Daftari; Mwanasiasa mkongwe na mbunge wa Uzini, Mohammed Seif Khatib; Profesa Makame Mbarawa ambaye pia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia; Yusuf Omar Mzee ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; na Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani.

Waliochaguliwa kutoka Bara ni Mwanasiasa mkongwe, Abdallah Kigoda, William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge; Stephen Wasira ambaye pia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais na Mahusiano na Uratibu, Mwansiasa mkongwe, Abdulrahaman Kinana; Mwanasiasa mkongwe Zakia Meghji, Pindi Chana na Constantine Buhebe ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera.

Rostam ambaye ni Mbunge wa Igunga na Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi walikuwa wajumbe wa CC iliyoundwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2007.

Kadhalika, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwateua kuwa wajumbe wa NEC katika nafasi za upendeleo makada wanane.

Waliochaguliwa ni Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo; Emmanuel Nchimbi; Mbunge wa Bumbuli, January Makamba; Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah, muasisi wa CCM, Peter Kisumo na Haji Omar.

Wengine walioteuliwa ni Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati, Zanzibar, Juma Ali Shamhuna, Katibu Mkuu Mstaafu, Wilson Mukama na Mbunge wa Iramba Magharibi, Lameck Mwigulu Mchemba

Katika hatua nyingine, NEC imewateua baadhi ya makada wa chama hicho kuwa wajumbe wa Sekretarieti yake.

Waliochaguliwa ni Wilson Mukama (Katibu Mkuu), John Chiligati (Naibu Katibu Mkuu Bara), Vuai Ali Vuai (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Nape Nnauye (Uenezi na Itikadi), Lameck Mugulu Mchemba (Fedha na Uchumi) na Asha Abdallah Juma (Oganaizesheni).

Mukama anayechukua nafasi aliyokuwa anaishikilia Yusuf Makamba, aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Chiligati anayechukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na George Mkuchika, alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa sekretarieti iliyopita. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Hivi sasa ni Mbunge wa Manyoni Mashariki.

Kabla kuchaguliwa kushika nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Ramadhan Ferouz, Vuai Ali Vuai alikuwa Katibu wa Uenezi Zanzibar.

Nape anayechukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Chiligati, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Asha abdallah Juma ambaye ni Waziri wa zamani wa Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana Zanzibar, anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Kidawa Saleh.

Mchemba anajaza nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla.

JK: MAFISADIWAJIWAJIBISHE

Hatua ya kwanza ni kuwabana watuhumiwa wawajibike wenyewe

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, amesema chama hicho kimeamua kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa vitendo vya utovu wa maadili.

Akifunga kikao cha NEC jana usiku mjini hapa, alisema hatua ya kwanza ni kuwabana watuhumiwa wawajibike wenyewe.

Rais Kikwete alisema hatua ya pili ni chama kuwawajibisha ikiwa watakataa kuwajibika wenyewe.

Tumekubaliana kwamba vitendo vya rushwa tunavichukia na tumeanza kuchukua hatua ili wenye kuhusishwa na vitendo vya rushwa wawajibishwe,” alisema na kuongeza:

Tumeanza safari ya kujenga upya chama chetu. Umoja wetu, mshikamano wake ndio utakaotufikisha mbele, kila mmoja atimize wajibu wake. Tumefanya maamuzi makubwa, na magumu lakini baridii.”

Alisema suala la utovu wa maadili ni miongoni mwa mambo ambayo yamekirudisha nyuma chama.

Hata hivyo, alisema hakuna moto uliowaka katika ukumbi wa mkutano na wajumbe walitoka bila unyonge na hakuna wa kumtumia mwenzake ujumbe fulani kwamba alimtukana.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Chiligati, alisema baada ya miezi mitatu wanachama ambao wanatajwa katika kashfa mbalimbali kama Richmond, Dowans EPA, Kagoda wawajibike.

Alisema hata kama hakuna ushahidi inatosha kwa chama kuwawajibisha.

CHANZO: NIPASHE

Baraza lapitisha bajeti bila madiwani wa Chadema Arusha

Baraza la Madiwani Jiji la Arusha limepitisha bajeti ya zaidi ya Sh. bilioni 48.1 kwa mwaka huu wa fedha wa 2011/ 2012, licha ya madiwani 11 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) kususia kikao hicho kilichofanyika jana kwa kutoka ukumbini.

Baraza hilo likiwa na wajumbe 16 kutoka vyama vya CCM na TLP, lililazimika kuendelea na kikao na kupitisha bajeti hiyo, huku baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kutoka vyama hivyo viwili wakishutumu hatua ya madiwani wa Chadema kususia kikao hicho.

Awali, baada ya wajumbe wote kuingia katika ukumbi, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomiah Chang’a, alitoa taarifa ya idadi ya madiwani waliokuwa ukumbini wakiwemo wa Chadema, CCM na TLP kuwa ni 25.

Alisema idadi hiyo ni zaidi ya akidi ya theluthi mbili ya wajumbe wote 32 wanaotakiwa kuhudhuria kikao hicho.

Lakini wakati Meya wa Jiji la Arusha, Mstahiki Gaudence Lyimo, aliposimama kwa ajili ya kufungua kikao hicho, madiwani wa Chadema wakiongozwa na John Bayo wa kata ya Elerai walinyanyuka vitini na kutoka nje ya ukumbi.

Hata hivyo, Chang’a, alisema kanuni na taratibu zinaelekeza kwamba iwapo mjumbe yeyote wa kuchaguliwa atapata wito na akaitikia na kufika ukumbini ni dhahiri mjumbe huyo atakuwa amehudhuria kikao hicho na hivyo kuchangia kufikia idadi ya wajumbe wanaotakiwa kufikisha akidi ya kikao ya theluthi mbili hata kama atakuwa ameondoka ukumbini.

Mbali na wadiwani wa Chadema kuingia ukumbini na kujiorodhesha katika kitabu cha mahudhurio, Bayo, aliamua kuchukuwa rejesta ya majina na kukatakata majina yao.

Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, Diwani wa TLP kutoka kata ya Sokoni One, Maiko Kivuyo, alisema wamepitisha bajeti ya jiji kwa manufaa ya wananchi wa Arusha.


CHANZO: NIPASHE

Upinzani waukataa muswada wa wafamasia bungeni

WABUNGE wa Kambi ya Upinzani wameupinga Muswada wa Sheria ya Wafamasia ya mwaka 2010 na kutaka urejeshwe katika Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ili ufanyiwe marekebisho zaidi.

Muswada huo uliowasilishwa bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, umeonekana kupingwa waziwazi na wabunge kutokana na mapendekezo yaliyomo ndani yake kuonekana kuwa na mapungufu. Muswada huo pamoja na mambo mengine unakusudia kuweka masharti ya kudhibiti na kusimamia taaluma na maadili ya wafamasia katika utoaji wa huduma huku ukilenga kuhamisha nguvu za Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) na kuzipeleka katika Baraza la Famasi.

Muswada huo uliosomwa kwa mara ya pili, unakusudia kufuta sheria namba moja ya mwaka 2003 ya mamlaka hiyo ili kuhamisha masharti yanayohusiana na taaluma ya famasi ambayo chini ya sheria hiyo yalikuwa yakisimamiwa na TFDA.

Chini ya muswada huo, Baraza la Famasi linapewa mamlaka ya kudhibiti na kusimamia taaluma na maadili ya wafamasia sambamba na usimamizi wa biashara ya dawa hususan utoaji wa leseni.

Aidha, wamelitaka Baraza la Famasi libaki na kazi ya kudhibiti na kusimamia taaluma na maadili ya wafamasia na suala la biashara libaki chini ya usimamizi wa TFDA.

Maoni ya kambi ya upinzani yaliyotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Dk. Gervase Mbassa, yaliweka wazi kuhusu msimamo wa kambi dhidi ya muswada huo.

“Muswada huu unataka kuweka utaratibu wa kusimamia taaluma na biashara ya famasi. Kambi ya upinzani inataka maelezo ya kina kabisa kwamba ni kwanini chombo cha kitaaluma kiwe chombo cha kusimamia biashara.

“Kambi ya upinzani ina shaka na muswada huu. Ni dhahiri huu muswada haujafanyiwa tafakuri ya kutosha na ni kama vile unataka kuridhisha kikundi kimoja katika jamii.

“Ni vema muswada huu urejeshwe kwenye kamati ili ukafanyiwe mabadiliko muhimu ya kuondoa vipengele vyote vinavyohusu usimamizi wa biashara ya famasi ili kutenganisha biashara na taaluma,” alisema Dk. Mbassa.

Akitilia nguvu hoja hiyo, Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Kabwe Zitto, alitaka kifungu cha nne cha muswada huo kiondolewe chote au muswada huo urejeshwe kwenye kamati.

“Baraza la Famasi libaki na kazi ya kusimamia taaluma na maadili tu halafu kazi ya kusimamia biashara waachiwe TFDA, huu muswada unafilisi majukumu ya TFDA ambayo hivi sasa ina uzoefu wa kutosha tangu mwaka 2003, iweje leo wapokonywe nguvu na Baraza?” alihoji Kabwe.

Naye Mbunge wa Vunjo Agustino Mrema (TLP) akichangia muswada huo alisema malengo ya muswada huo ni mazuri kwa kuwa pamoja na mambo mengine unalenga kudhibiti tatizo la wafamasia bandia.

Akisoma maoni ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kwa niaba ya Mwenyekiti, Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile (CCM), alisema kamati yake imeridhishwa na muswada huo.

“Kamati inaunga mkono hatua ya serikali ya kuleta muswada huu kwa lengo la kuwa na Baraza la Famasi, ambalo litakuwa na jukumu la kusimamia taaluma katika fani ya famasia.

“Pamoja na majibu ya waziri, kamati iliendelea kushauri kwamba kifungu cha 37 (1) (b) kiangaliwe upya, ili jukumu la utoaji wa leseni za uingizaji wa dawa na utengenezaji wa dawa nchini libaki kuwa la TFDA,” alisema Dk. Ndugulile


SOURCE TANZANIA DAIMA

Sunday, March 6, 2011

Sumaye: CCM ijibu hoja za Chadema

WAKATI CCM ikitaka dola ikidhibiti Chadema, Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya tatu, Fredrick Sumaye, amekitaka chama hicho tawala kukabiliana na hoja za Chadema kisiasa badala ya kuiachia Serikali ipambane nao.Juzi CCM kilisema nyendo za Chadema zina agenda ya siri ya kuking’oa madarakani kwa kutumia nguvu kinyume cha katiba hivyo kiliitaka Serikali na vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria haraka.

“CCM inaviomba vyombo vya dola viwe imara kuchukua hatua za kisheria… Wanachofanya Chadema ni kutuchonganisha na wananchi, kutoa kauli hatari za kujaribu kughilibu akili za watu ili kuchochea machafuko, umwagaji wa damu na uasi. “Wanachochea wananchi wakisema, ‘peoples’ na hujibu ‘power’! (nguvu ya umma), Je mpo tayari kufanya kama Tunisia, Misri? (ambako serikali zilipinduliwa kwa nguvu ya umma)” alisema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika juzi, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili bila kujua kwamba CCM wangekuwa wanazungumzia suala hilo, Sumaye alisema CCM inatakiwa kukabiliana kisiasa na hoja za Chadema na si kuiachia Serikali ipambane nao.

Kwa mujibu wa Sumaye, kazi ya siasa ni ya chama na si serikali, hivyo CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na Chadema kwa sera na kujibu hoja zao zote ili kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho.Sumaye alisema si ishara nzuri kwa CCM kukaa kimya wakati wapinzani wanaendelea kukishtaki kwa wananchi kuwa kimeshindwa kufanya kazi.

Sumaye ambaye Mwananchi Jumapili ilimtafuta kusikia maoni yake kuhusu mfululizo wa mikutano ya Chadema na mustakabali wa CCM, alisema chama hicho tawala kinapaswa kujibu hoja zote za Chadema kisiasa na kama hakina majibu kiiombe Serikali majibu hayo na iyatoe kwa wananchi.

“Wale (Chadema) wanafanya kazi za siasa na hawa (CCM) wamekaa kimya, wanaiachia Serikali ndio inatoa majibu, hali hiyo si nzuri, chama kinapaswa kujibu hoja zote na kama hakina majibu, kiombe kwa serikali,” alisema Sumaye.Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia taifa kupitia radio na televisheni Februari 28, mwaka huu na kuwaleza wananchi kuwa chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini.

Rais Kikwete alisema hayo alipokuwa akilihutubia taifa mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.Kauli hiyo ya Rais Kikwete ambaye Chadema waliipuuza, ilisisitizwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira, aliyesema kuwa Chadema wasije kuilaumu serikali ikikosa uvumulivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.

Akihojiwa na gazeti hili Sumaye hakuishia kuishauri CCM kuja na hoja za kisiasa kujibu mapigo ya Chadema, bali pia alieleza aina ya watu wanaofaa kukiongoza chama hicho tawala wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kisiasa.Sumaye alisema CCM inahitaji viongozi waadilifu, wachapakazi na wasio waoga kumshauri rais ili kuwa na mabadiliko ya kiutendaji yanayoendana na joto la kisiasa lililopo. “Tunahitaji viongozi wasioogopa kumshauri rais juu ya masuala mbalimbali, kama utakuwa na viongozi waoga, lazima kutakuwa na matatizo,” alisema Sumaye.

Kuhusu mabadiliko ndani ya CCM ambayo Rais Kikwete alisema ni lazima yafanyike, Sumaye alisema anakubaliana msimamo huo na anampongeza Rais kwa kutambua kuwa chama kinahitaji mabadiliko makubwa ya kiutendaji.“Kwanza nampongeza Mwenyekiti, maana ameona hilo. Watu wengi wanaona kuna umuhimu chama kurekebishwa na eneo muhimu ni utendaji wa viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama,” alisema Sumaye.

Sumaye alieleza kuwa CCM kitaendelea kushika dola, lakini kama kinataka hayo yatimie, mabadiliko ndani ya chama ni muhimu.Alisema umuhimu wa CCM kujifanyia tathmini ya utendaji ulianza kujionyesha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambapo ikilinganishwa na chaguzi nyingine, chama kilipata upinzani mkali."Sasa ni dhahiri kunahitajika mikakati madhubuti ili kuhakikisha mwaka 2015 unakuwa mrahisi kwa CCM," alisema Sumaye.

Ndejembio atabiri anguko
Habel Chidawali anaripoti kutoka Dodoma kuwa, Kada maarufu wa CCM, Pancras Ndejembi amekitabiria chama hicho kikongwe kuzama.Kada huyo ambaye ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma alisema jana kuwa hali ilipofikia kwa sasa, CCM inaonekana kupoteza mwelekeo na kutia shaka mustakbali wa chama hicho siku za usoni.

Ndejembi ambaye aliwahi kutumikia nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali na chama katika utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza, alisema CCM bado haijaingia shimoni ila inaelekea huko.“Ni kweli chama hakifuati utaratibu uliokuwepo ndio maana nasema kuwa kinaelekea kuzama tofauti kabisa na enzi zetu ambapo Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anasisitiza kuwa turudi kwa wanachama tukae nao na kuzungumza, jambo ambalo sasa hilo halipo na viongozi wamebaki huko juu,” alisema Ndejembi.

Alisema viongozi wa ngazi ya taifa wamebaki katika maofisi yao na kushindwa kurudi katika ngazi za chini kuimarisha chama na matokeo yake wanaishia kupiga kelele bila ya kuwa na uhakika wanachama ngazi ya chini wanataka nini.Ndejembi hivi alisema hakuna mshikamano wa dhati ndani ya chama jambo linalowafanya wanachama kumuachia mzigo wote Mwenyekiti wa Taifa.

“Watu wanaishia kulaumiana kila kona kwamba chama kimefanya nini, mara wanasema bado kimesimama wengine wanasema kuwa kinayumba, ila ukweli utabaki palepale kuwa CCM tunazama sasa,” alisisitiza.Kuhusu nguvu ya wazee ndani ya Chama Ndejembi alisema: “Sisi tumestaafu hivyo tupo tupo na kama hawataki kutuita unadhani tutakwenda ? Lakini, wakisema tuende tuko tayari kukaa pamoja nao kutengeneza utaratibu wa kukinusuru chama kisizame kabisa katika tope”.Ushauri

Kuhusu nini kifanye ili kukinusufu CCM, alisema unahitajika mshikamano wa dhati kati ya viongozi na wanachama: “viongozi wanahitaji kutambua kwa dhati kuwa chama kiko ngazi ya chini kuanzia kwa wajumbe wa nyumba kumi sio ngazi ya mikoa”.Alishauri kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa anatakiwa abaki kama kiongozi wa kutoa ushauri kwa juu, lakini awe na watu wanaochukua mawazo kutoka kwa wanachama wa ngazi ya chini.

Hata hivyo, alisema viongozi wa taifa bado wana mfumo mbovu wa mawasiliano, kwani kila mtu katika nafasi ya juu ni msemaji, jambo linalofanya wajichanganye katika taarifa zao.

SOURCE. MWANANCHI

Saturday, March 5, 2011

maandamano ya CHADEMA Mjimbo la chato




wakazi wa chato na vitongoji vyake wajitojeza kwenye maandamano a CHADEMA
.

chumba kimoja madarasa mawili






UHABA wa vyumba vya madarasa umewalazimu wanafunzi wa madarasa tofauti katika Shule ya Msingi Magwalasi iliyoko Kata ya Rujewa wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya kusoma katika chumba kimoja kwa kugeuziana migongo.

Waandishi wa habari walifika hapo jana na kukuta shule hiyo yenye wanafunzi 269 na walimu saba wa kuanzia chekechekea, darasa la kwanza hadi la saba ikiwa na vyumba vinne pekee vya madarasa.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Jonathan Chengula aliwaambia waandishi wa habari kuwa katika shule hiyo iliyoanza na kusajiliwa mwaka 2003, wanafunzi wa darasa la kwanza wanasoma chumba kimoja kwa wakati mmoja na wale wa chekechea, darasa la pili wanasoma pamoja na wenzao wa darasa la tatu, la sita na la tano, huku wale wa darasa la saba wakitumia chumba kimoja na wa darasa la nne.

“Tatizo kubwa ambalo linatusumbua katika shule yetu ni upungufu wa madarasa. Tuna madarasa manne tu hivyo imetulazimu kuweka mbao za kufundishia mbili katika chumba kimoja ili madarasa mawili yaweze kutumia kwa wakati mmoja,” alisema.

Kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo, ili kukabiliana na upungufu huo wa madarasa na kutokana na mazingira ya shule hiyo, ndiyo maana wameramua wanafunzi wa madarasa mawili tofauti wasome katika chumba kimoja kwa kugeuziana migongo kwa maana ya kuwa wengine wanageukia upande wa kulia na wengine kushoto.

“Kama mnavyowaona hawa waliogeukia huko ni darasa la saba na hawa wengine ni darasa la nne na katika darasa hili jingine wanasoma darasa la pili na tatu ndivyo tunavyo kwenda," alisema.Alisema kuwa mwalimu wa darasa la saba anapoingia kufundisha, wa darasa la nne anasubiri mwenzake amalize huku wanafunzi hao wa darasa la nne wakiwemo humo humo ndani wakisikiliza wale wa darasa la saba wanavyofundishwa.

Alisema wakati mwingine walimu huamua kuwatoa nje na kuwaweka chini ya mti kama umefika wakati wa kusoma kitabu cha Kiswahili ili wasome wakiwa nje na wengine waendelee na masomo.

Mwalimu aliyekuwa darasani akifundisha, Shufaa Ramadhani alisema mazingira hayo ya ufundishaji ni magumu kwani kuna athari kubwa kwa wanafunzi na upande wa mwalimu kwani kufundisha wote kwa pamoja pia ni vigumu.

Alisema kuwa utaratibu huo unawaathiri watoto kisaikolojia kwani kuna uwezekano wa kusahau yale ambayo wamefundishwa na mwalimu wao na badala yake kusikia ya upande wa pili ambayo ni masomo ya darasa jingine ambalo tayari walishayapitia au bado hawajapitia.

Mwalimu Shufaa alisema walimu wanaathirika kwa kupoteza vipindi vingine kwa mujibu wa uandaaji wa masomo na vipindi kwani inamlazimu asubiri mwenzake amalize kufundisha na ndipo aingie na kufundisha somo lake.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, George Kagomba hakupatikana kuzungumzia tatizo hilo na alipotafutwa kwa simu alijibu kuwa yuko kwenye kikao cha maandalizi ya Mbio za Mwenge.

Mkurugenzi huyo aliwataka waandishi kwenda kwa Ofisa Elimu wa Wilaya ya Mbarali. Hata hivyo, aliyekuwa akikaimu ofisi hiyo hakuwepo. Ofisa elimu wa Wilaya alikuwa amesafiri kikazi.

SOURCE MWANANCHI

Friday, March 4, 2011

anti government protests in libya





































waziri mkuu wakiwa kwenye ziara yake huko kagera.



waziri mkuu ananza ziara yake huko mkoani kagera kwa ajili ya kufungua na kuzindua huduma za maendeleo katika mkoa huo

SPEECH BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE 5TH GLOBAL CONFERENCE OF THE EXRTRACTIVE INDUSTRIES TRANSPA

Madam Clare Short, Plenary Chairman;

Mr Peter Eigen, Chairman of EITI;

Excellencies Heads of State and Government present here today;

Distinguished Participants;

Ladies and Gentlemen;

Good morning!

Madame Chairman;

Since I am participating in this important global conference for the first time, allow me to thank Mr. Peter Eigen, The Chairman of EITI for the kind invitation. It is a great honour for me and my country. Allow me also to express my deepest thanks and appreciation to the Board of EITI for accepting Tanzania’s application for membership of the EITI.

I took the decision for Tanzania to join the EITI after appreciating the benefits my country would get from being a member. I am happy with the progress we have made so far in the process towards full membership. I wish we could get there earlier. But I appreciate your support and cooperation.

Abundant Natural Resources

Ladies and Gentlemen;

Tanzania is richly endowed with natural resources such as minerals, gas, forestry, fishing etc. So far exploitation of minerals, particularly gold and gemstones as well as natural gas, is the most significant of them all. At an average growth rate of 12.4 percent for the past decade, mining is one of the fastest growing sectors of the Tanzanian economy. Unfortunately, mining accounts for a meagre 2.3 percent of the GDP but contributes a significant one-third of foreign exchange earnings for the country.


Mineral Audit

Ladies and Gentlemen;

Mining, therefore, is a critically important sector for Tanzania’s economic prosperity, now and in the future. There are still abundant opportunities yet to be explored and exploited. In recent years our pre-occupation has been about how to ensure that the nation, through the government, benefits equitably from mining activities.

Accountability and transparency on the part of mining operations were matters of essence. We undertook a comprehensive review of the mineral sector, in the country, where these factors were underpinned in our new Mineral Policy and the new Mining Law. You may be delighted to know that the person who chaired the Mineral Sector Review Commission, that I set up in 2007, Judge Mark Bomani is the Chairman of the Multi-Stakeholder Working Group of the Tanzania EITI chapter.


Ladies and Gentlemen;

Prior to that, and, in the spirit of promoting accountability and transparency, mineral audit was introduced to enable the government monitor operations of mining companies. At the beginning this service was outsourced from abroad and, in 2007 we established the Tanzania Mineral Audit Agency manned by Tanzanian nationals. The mandate of the Agency was to monitor investments, costs of operations, and revenues of mining companies as well as payment of government taxes and loyalties.

Ladies and Gentlemen;

The introduction of mineral audit facilitated availability and verification of information about the operations of mining companies in Tanzania. Before that, mining companies were the only source of information and there was nobody to ascertain the veracity of the information. As such, everything simply depended on the integrity and trustworthiness of company officials.

Under such circumstances, the danger of companies not telling the truth and the risk of our mineral resources being depleted without companies paying the proper taxes was real. There was a genuine fear that we would lose all our minerals to the investors and get very little or nothing at all in return. To date, because of the good work being done by Tanzania Mineral Audit Agency, we can confidently say that things have began to change and will continue to change for the better. There is greater transparency and accountability now, than was the case before. It has become easier these days for the government to know how much to collect in the form of taxes and loyalties from mining companies.

Implementing EITI Principles

Ladies and Gentlemen;

Our membership of the EITI has complimented well the efforts we had begun. EITI has been a great inspiration, indeed. In fact, it has strengthened our hand and resolve in the quest for accountability and greater revenue transparency in the exploitation of our natural resources. Although the EITI is a new initiative in Tanzania, it is already showing positive results. It has taken our efforts a step further.

In February, 2011 Tanzania published its first EITI report detailing payments made by mining companies to the Government from the period of July 1, 2008 to June 30, 2009. The report is playing a useful role in informing the Tanzanian public about revenues generated from the extractive industries. Rightly so, its publication and release has generated public and parliamentary discussions about the role of government in revenue collection and the contribution of the mineral sector to our economy.

Ladies and Gentlemen;

A number of important issues were raised in the report which the government is now following up in order to resolve them. For example, we have assigned the Controller and Auditor General (CAG) to examine the reported discrepancies in various payment transactions between mining companies and government agencies. About USD 36 million is reported to be involved in this case.

Ladies and Gentlemen;

Tanzania is proud to be part of EITI global family and, to be among the countries implementing the EITI principles and values. We are committed to the EITI process because it is aligned with our policy of promoting transparency and accountability in the management and use of our natural resources. It is critical for promoting sustainable development and poverty eradication in the country.

Ladies and Gentlemen;

I am confident that implementing the EITI principles and values, to the letter and spirit, will encourage compliance on the part of all stakeholders. They will all know that there are some people somewhere who are watching with very keen eyes. It will also help build trust among Tanzania’s public and reduce their scepticism about the role and contribution of the extractive sector in their socio-economic well-being. And, if, the practise of corporate social responsibility is observed, more trust will be engendered between investors and the people living around the mining operations because both of them will be benefiting.

Certainly, implementing EITI principles and values will go a long way towards enabling countries benefit equitably from their natural resources which God generously endowed on them. It will make resources be an opportunity rather than become a curse and source of conflicts as it has happened on some mineral-rich countries in Africa.

Conclusion

Ladies and Gentlemen;

It would be remiss of me if I concluded my remarks without acknowledging and thanking members of the Tanzania Multi-stakeholder Group, the International EITI Secretariat, the World Bank, the African Development Bank, Norway, Canada and the UK for their support to the Tanzania EITI process. We have come so far because of their invaluable support. I am grateful and all Tanzanians are grateful. Please, lets continue to work together.

Once again, I would like to reaffirm Tanzania’s commitment to the EITI principles, standards and values.

Thank you for listening.

Govt: We are fed up with embezzlers of donor funds

he government has said it would no longer tolerate a few people misusing funds provided by donors for community development projects in the country.

Speaking at a recent signing of a grant agreement between the governments of Japan and Tanzania, deputy minister in the Prime Minister's Office (Regional Administration and Local Governments) Aggrey Mwanri said his office would tighten control measures to ensure that funds provided by donors were put to the intended use.

He said his office would be visiting all projects being implemented by using donors’ funds to make sure that the money was spent according to their intended purposes.

Japan extended a 462m/- grant to Tanzania for three educational and health projects in Iramba, Namtumbo and Same districts.

In his remarks at the ceremony, Japanese Ambassador to Tanzania Hiroshi Nakagawa said his office has decided to provide funds under the Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects in response to basic needs at the grassroots level in the country.

He said the money would be spent on the construction of girls’ hostels at Oshara Secondary School in Siha District, Kilimanjaro Region, and Nanungu Secondary School in Namtumbo District, Ruvuma Region.

The rest of the money, he said, would be spend on the third project, which is the construction of a new dispensary in Iramba District, Singida Region.

“Education is a basic need for human beings; it provides knowledge and skills for the social and economic development of a nation. Finally, it provides quality life to the people,” said the envoy.

Iramba West member of Parliament Mwigulu Madelu said that the grant to his constituency had been extended at the right time because it would assist people, especially pregnant women currently trekking long distances looking for treatments, to get the services not far from their homes.

He said his office would work closely with the district council to make sure that funds meant for putting up a new dispensary were wisely and properly spent.

SOURCE: THE GUARDIAN

source Mwananchi, Pinda kufanya ziara kanda ya ziwa

KATIKA kile kinachoonekana kama mpango wa Serikali kukabiliana na nguvu za maandamano na mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo anatarajiwa kuanza ziara ya siku nane katika Mkoa wa Kagera ambako atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kutembelea wilaya zote za mkoa huo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Waziri Mkuu ataanzia ziara yake katika Manispaa ya Bukoba kisha atakwenda Muleba, Chato, Biharamulo, Ngara, Karagwe, Missenyi na kumalizia Bukoba Vijijini.

Katika ziara yake ya Kanda ya Ziwa, Chadema kilitembelea na kufanya mikutano katika Wilaya za Biharamulo, Misenyi, Muleba na Chato ambako viongozi wake walifanya mikutano na maandamano huku wakitaka Kampuni ya kufua umeme ya Dowans isilipwe, bei ya umeme ishuke na kikitaka utawala wa CCM uwajibike.

Baadhi ya shughuli kubwa ambazo Waziri Mkuu amepangiwa kufanya wakati wa ziara hiyo ni pamoja na kuzindua Barabara ya Zamzam na mkutano wa hadhara kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba katika Uwanja wa Mayunga (Uhuru Platform).

Akiwa wilayani Muleba, Waziri Mkuu Pinda atakagua shamba la mkulima bora wa kahawa katika Kijiji cha Ilogero kabla ya kwenda Buganguzi ambako atakagua mashamba ya migomba yaliyoshambuliwa na magonjwa ambayo mpaka sasa hayajajulikana kisayansi.

Pia ataweka jiwe la msingi katika mradi wa umwagiliaji katika Kijiji cha Buyaga na kuhutubia wananchi katika Viwanja vya Shule ya Msingi ya Kasharunga.

Akiwa wilayani Chato, Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kufungua Saccos ya Mshikamano kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Shule ya Msingi Chato.

Akiwa Biharamulo, Waziri Mkuu atakagua mnada wa ng’ombe wa Lusahunga, kukagua ujenzi wa wodi katika hospitali hiyo na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya St Clara huko Rukaragata na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Michezo wa CCM.

Akiwa Biharamulo, Jumanne ijayo Waziri Mkuu atakwenda Ngara kufungua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Ngara Farmers kabla ya kwenda kwenye Mgodi wa Nickel wa Kabanga. Pia atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara huko Muurusagamba.

Akiwa Karagwe, Jumatano ijayo atakagua bwawa la samaki huko Kishoju na kusalimiana na wananchi kisha atakwenda Kayanga kuzindua jengo la masjala ya ardhi. Mchana ataweka jiwe la msingi katika Chuo cha Ualimu Katera kabla ya kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Isingiro.

Akiwa Missenyi, Alhamisi ijayo, Waziri Mkuu ataweka jiwe la msingi katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo. Baadaye ataelekea Kiwanda cha Sukari cha Kagera kuona mitambo ya kisasa ya umwagiliaji mashamba ya miwa. Pia atakagua shughuli za kiwanda hicho na kisha kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa Mashujaa wa Bunazi.

Akiwa Bukoba Vijijini, Ijumaa, Waziri Mkuu atatembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku, maabara na baadhi ya vijishamba vya utafiti wa kilimo. Pia atakwenda Hospitali ya Izimbya kuzindua majengo ya OPD, watoto, maabara, chumba cha upasuaji na jengo la ushauri na upimaji VVU (CTC).

Jumamosi ijayo, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu Mkoa na kurejea jijini Dar es Salaam mchana huo.


Mbunge wa Jimbo la Vunjo, mwenyekiti wa Chama cha TLP na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali za Mitaa Dk. Augustino Lyatonga Mrema akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa angalizo kwa chama cha CHADEMA kutokana na mikutano yake inayohamasisha maandamano akisema kuhamasisha maandamano kunaweza kuleta uvunjifu wa amani kama ilivyotokea kwa nchi za Madagascar, Misri, Tunisia na sasa Libya. Dk. Mrema ameongeza kwamba kwa kawaida mkiiangusha serikali bila kufuata utaratibu wa kikatiba upo uwezekano mkubwa wa kuleta vurugu katika nchi kama ilivyotokea kwa nchi hizo za kiafrika ambazo hata walipoondolewa watawala ambao walikuwa hawatakiwa bado hakuna utulivu na mahali pengine jeshi limepata mianya ya kuchukua madaraka kwa lengo la kuhakikisha usalama wa nchi zao kama ilivyotokea kwa Misri ambayo kwa sasa inaongozwa na Jeshi, katika picha kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Mh. Hamad Tao.

Thursday, March 3, 2011

VIWANGO VIPYA VYA JUU VYA NAULI ZA MABASI YA DALADALA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM


Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini husan katika Jiji la Dar es Salaam. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 10 Machi, 2011.

Katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka wa fedha wa 2009/2010, SUMATRA ilipokea maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara wakiwemo Umoja wa Wamiliki wa Daladala (DARCOBOA) wakipendekeza mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini (Daladala) kufuatia ongezeko la gharama za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao. Maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya nauli kwa kati ya 172% na 200% ya viwango vya sasa.

Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRA iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.

Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti, haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA imeamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za Daladala kwa wastani wa 17.9% ambapo kiwango cha nauli kwa abiria kwa kila kilomita kimepanda kutoka Sh 22.9 hadi Sh 27.

Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo:

1. Nauli za Daladala – Jiji la Dar es Salaam

Umbali wa Njia

Kiwango Kipya cha Nauli

Mfano wa Njia

Kilomita kati ya 0 – 10

Sh 300

Mbagala – Posta

Kilomita kati ya 0 - 15

Sh 350

Kawe - Kariakoo

Kilomita kati ya 0 - 20

Sh 400

Kimara – Posta

Kilomita kati ya 0 - 25

Sh 500

Tegeta - Kariakoo

Kilomita kati ya 0 - 30

Sh 650

Kibamba - Kariakoo

Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 150/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 300/=. Nauli hii itatumika kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam .

Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:

(i) Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria

(ii) Kuandika katika mlango wa kuingia abiria viwango vya nauli inavyotoza katika njia anayotoa huduma ya usafiri

(iii) Kutoa tiketi kwa kila abiria ikionyesha jina la mmiliki, namba ya usajili wa basi, kituo cha mwanzo na mwisho wa safari, nauli na tarehe ya safari

(iv) Kuzingatia usafi wa mabasi na sare za wafanyakazi wao, kutotumia wapiga debe, kutotumia lugha chafu, kutokatisha njia na kutowabugudhi wanafunzi

(v) Kubeba idadi ya abiria kulingana na uwezo wa basi na kuwepo na nafasi ya kutosha na sehemu ya kushika kwa abiria wanaosimama ndani ya mabasi makubwa

(vi) Kuhakiksha basi linabeba idadi ya abiria ambao wanapaswa kubebwa kwa mujibu wa idadi iliyoidhinishwa na mtengenezaji wa basi

(vii) Kuwepo na Bima inayowalinda abiria wote wa basi husika

(viii) Abiria wanawajibika kurejesha utamaduni wa kupanga mabasi kwa mstari na mabasi nayo yanapaswa kupakia abiria kwa mstari.

Ni vyema ikumbukwe kuwa SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji. Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe.

Mamlaka ya SUMATRA inaendelea kuimarisha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka zingine kama Ofisi ya Mkuu wa Mikoa, Serikali za Mitaa, Mamlaka za Manispaa, Polisi, TBS, TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi kwa ujumla, katika kuleta mageuzi ya utoaji wa huduma za usafiri wa barabara kwa kiwango cha juu.

Imetolewa na:

David Mziray

Meneja Mawasiliano kwa Umma

3 Machi, 2011